Anayeswali peke yake anakata swalah ili ajiunge na wanaoswali mkusanyiko

Swali: Mtu alikuwa anaswali swalah ya faradhi peke yake na wakati huohuo wakaingia watu msikitini wakaanza swalah ya mkusanyiko. Je, akate swalah yake au ainue nia yake iwe ni ya sunnah ili aswali pamoja nao?

Jibu: Lililo bora ni kuigeuza swalah yake iwe sunnah kisha aswali pamoja na wale walioingia kwa swalah ya mkusanyiko ili apate fadhilah ya swalah ya mkusanyiko. Kama akiikata kisha akaswali pamoja nao pia hakuna ubaya, kwa sababu ameikata kutokana na maslahi ya Kishari´ah yanayorudi katika swalah yenyewe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/155)
  • Imechapishwa: 07/03/2026