Swali: Ni ipi hukumu ya yule anayemkuta imamu akiwa katika Rukuu´. Je, amewahi Rak´ah? Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Swalah haisihi pasi na Ufunguzi wa Kitabu.”?
Jibu: Sahihi ni kwamba ikiwa amemkuta imamu katika Rukuu´ basi huhesabiwa kuwa ameipata Rak´ah. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuja Abu Bakrah ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) akiwa katika Rukuu´, alirukuu pamoja naye nje ya safu kisha akaingia katika safu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
“Allaah akuzidishie pupa, lakini usirudie tena.”[1]
Hakuamrishwa kuilipa Rak´ah hiyo, jambo ambalo likafahamisha ya kwamba ni mwenye udhuru. Hivyo basi Hadiyth yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakuna swalah kwa yule ambaye hakusoma Ufunguzi wa Kitabu”[2]
ni maneno ya jumla kwa imamu na anayeswali peke yake. Kwa hiyo imamu au anayeswali peke yake akiiacha, basi ni wajibu kwake kuirudia swalah ikiwa muda umepita mrefu. Ikiwa muda haujapita mrefu, ataswali Rak´ah moja badala ya ile Rak´ah ambayo hakusoma al-Faatihah. Kisha atasujudu sijda ya kusahau ikiwa hilo lilitokea kwa kusahau. Lakini ikiwa aliiacha kwa makusudi, basi ataikariri swalah kwa hali zote kwa sababu swalah yake inakuwa batili.
[1] al-Bukhaariy (783).
[2] al-Bukhaariy (756) na Muslim (394).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/154)
- Imechapishwa: 06/03/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya yule anayemkuta imamu akiwa katika Rukuu´. Je, amewahi Rak´ah? Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Swalah haisihi pasi na Ufunguzi wa Kitabu.”?
Jibu: Sahihi ni kwamba ikiwa amemkuta imamu katika Rukuu´ basi huhesabiwa kuwa ameipata Rak´ah. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuja Abu Bakrah ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) akiwa katika Rukuu´, alirukuu pamoja naye nje ya safu kisha akaingia katika safu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
“Allaah akuzidishie pupa, lakini usirudie tena.”[1]
Hakuamrishwa kuilipa Rak´ah hiyo, jambo ambalo likafahamisha ya kwamba ni mwenye udhuru. Hivyo basi Hadiyth yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakuna swalah kwa yule ambaye hakusoma Ufunguzi wa Kitabu”[2]
ni maneno ya jumla kwa imamu na anayeswali peke yake. Kwa hiyo imamu au anayeswali peke yake akiiacha, basi ni wajibu kwake kuirudia swalah ikiwa muda umepita mrefu. Ikiwa muda haujapita mrefu, ataswali Rak´ah moja badala ya ile Rak´ah ambayo hakusoma al-Faatihah. Kisha atasujudu sijda ya kusahau ikiwa hilo lilitokea kwa kusahau. Lakini ikiwa aliiacha kwa makusudi, basi ataikariri swalah kwa hali zote kwa sababu swalah yake inakuwa batili.
[1] al-Bukhaariy (783).
[2] al-Bukhaariy (756) na Muslim (394).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/154)
Imechapishwa: 06/03/2026
https://firqatunnajia.com/anayejiunga-na-imamu-katika-rukuu-amewahi-rakah/