Swali: Kauli ya anayesema:
“Mwenye kumuabudu Allaah kwa mapenzi pekebaaze amefanya uzandiki.”
inamaanisha nini?
Jibu: Ni lazima kuwe na mapenzi pamoja na matendo, kwani mapenzi ya kweli humpelekea mtu kutenda. Allaah amesema:
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ
“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah.”[1]
Kwa hiyo wale wanaodai kumpenda Allaah lakini hawatendi matendo ya utiifu ni wazindiki; wanadai mapenzi bila ukweli. Lau kweli wangempenda Allaah, wangelitenda:
Je, wampenda maadui wa mpenzi na huku unadai kumpenda yeye?
Hilo haliwezekani!
Kwa hiyo mapenzi ya kweli yanamfanya mtu atende kwa utiifu kwa Allaah na aache maasi Yake. Ikiwa hatendi hivyo, basi madai yake ya kumpenda Allaah ni uongo.
[1] 03:31
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31143/ما-معنى-ان-من-عبد-الله-بالمحبة-وحدها-تزندق
- Imechapishwa: 06/10/2025
Swali: Kauli ya anayesema:
“Mwenye kumuabudu Allaah kwa mapenzi pekebaaze amefanya uzandiki.”
inamaanisha nini?
Jibu: Ni lazima kuwe na mapenzi pamoja na matendo, kwani mapenzi ya kweli humpelekea mtu kutenda. Allaah amesema:
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ
“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah.”[1]
Kwa hiyo wale wanaodai kumpenda Allaah lakini hawatendi matendo ya utiifu ni wazindiki; wanadai mapenzi bila ukweli. Lau kweli wangempenda Allaah, wangelitenda:
Je, wampenda maadui wa mpenzi na huku unadai kumpenda yeye?
Hilo haliwezekani!
Kwa hiyo mapenzi ya kweli yanamfanya mtu atende kwa utiifu kwa Allaah na aache maasi Yake. Ikiwa hatendi hivyo, basi madai yake ya kumpenda Allaah ni uongo.
[1] 03:31
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31143/ما-معنى-ان-من-عبد-الله-بالمحبة-وحدها-تزندق
Imechapishwa: 06/10/2025
https://firqatunnajia.com/anayedai-kumwabudu-allaah-kwa-mapenzi-pekee-ni-zandiki/