Anataka kuswalishwa na ambaye anaswali peke yake

Swali: Mtu akimuona mswaliji anaswali peke yake ajiunge naye? Je, amuulize kama anaswali swalah ya faradhi au swalah ya kujitolea? Atajibu vipi?

Jibu: Inafaa ukajiunga na mtu anayeswali peke yake na ukanuia akuswalishe. Hakuna haja kumuuliza anachoswali. Wewe utajiunga na nia ya kuswali ulichokusudia. Ikiwa swalah yake inaafikiana na swalah yako ni vyema. Vinginevyo ikamilishe swalah yako kutokana na vile ulivyonuia. Baadaye ikibaini kuwa yeye anaswali ´Ishaa na wewe umenuia Maghrib na umejiunga naye katika ile Rak´ah ya kwanza, ataposimama katika ile Rak´ah ya nne basi keti chini ulete Tashahhud na utoe salamu. Baadaye jiunge naye katika ile sehemu iliyobaki ya ´Ishaa ikiwa inakujuzukia kukusanya swalah. Kuhusiana na kumuuliza kitu anayeswali, hapana vibaya akakujibu kwa kuashiria.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/446)
  • Imechapishwa: 12/04/2026