Anataka kufungua swawm anayolipa ya Ramadhaan

Swali: Je, inampasa kukamilisha swawm ikiwa mfungaji analipa masiku yake ya Ramadhaan kisha akataka kufungua na kufunga siku nyingine badala ya siku hii?

Jibu: Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba ameshaanza ´ibaadah ya faradhi na hivyo inampasa aikamilishe. Haijuzu kwake kufungua isipokuwa kutokana na udhuru, kama ugonjwa uliompata, safari au tukio jingine. Vinginevyo ni wajibu kwake kukamilisha swawm ya faradhi kama kulipa Ramadhaan au nadhiri. Aikamilishe na asifungue isipokuwa kwa sababu inayomruhusu kufungua.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1247/حكم-من-شرع-في-صيام-القضاء-ثم-اراد-ان-يفطر
  • Imechapishwa: 08/02/2026