Swali: Mtu akichelewesha Dhuhr mpaka wakati wa ´Aswr na akaingia msikitini. Je, aswali nao ´Aswr kwa nia ya Dhuhr?
Jibu: Hakujabainishwa katika swali sababu ya kuchelewesha Dhuhr mpaka wakati wa ´Aswr. Ikiwa kuchelewesha kunatokana na udhuru wa Kishari´ah, basi kuna hukumu yake. Ikiwa kuchelewesha ni pasi na udhuru unaokubalika Kishari´ah, basi kuswali Dhuhr hakusihi akiichelewesha nje ya wakati wake. Katika hali hiyo ni lazima kwake kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) juu ya dhambi yake. Aidha swalah yake haisihi kwa sababu ameichelewesha kwa makusudi mpaka ukatoka wakati wake.
Lakini ikiwa ucheleweshaji ni kwa sababu ya Kishari´ah na akaja msikitini na akakuta wanaswali ´Aswr, basi anayo khiyari akitaka ataswali ´Aswr pamoja nao na wakimaliza ataswali Dhuhr, kwa maana hiyo atakosa kule kupangilia swalah kwa sababu asije kukosa swalah ya mkusanyiko, na akitaka ataswali nao ´Aswr kwa nia ya Dhuhr. Haimdhuru kitu kule kutofautiana kwa nia, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika hapana vyengine imamu amewekwa ili afuatwe. Hivyo basi, msitofautiane naye. Akienda katika Rukuu´, nanyi rukuuni.”[1]
Bi maana msitofautiane naye katika matendo. Hayo yamefasiriwa katika Hadiyth hiyohiyo, pale aliposema:
“Akienda katika Rukuu´, nanyi rukuuni.”
Kuhusu nia ni kitendo kilichojificha ambacho hakionekani kwa imamu. Kwa msemo mwingine mtu huyo ajiunge nao kwa nia ya Dhuhr ijapo wao wanaswali ´Aswr; kisha wakimaliza kuswali aswali swalah ya Dhuhr kivyake. Naona kuwa hili la pili ndio bora zaidi kuliko lile la mwanzo.
[1] al-Bukhaariy (722) na Muslim (417).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/451-452)
- Imechapishwa: 20/03/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/451-452)
Imechapishwa: 20/03/2026
https://firqatunnajia.com/anaswali-dhuhr-nyuma-ya-imamu-anayeswali-aswr/