Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mwenye kusikia adhaana naye yuko usingizini, akajaribu kusimama kwa ajili ya swalah lakini usingizi na uvivu vikamshinda. Baada ya watu kumaliza kuswali akasimama na kuswali nyumbani kwake peke yake?
Jibu: Haya ni maovu. Haijuzu kwake kufanya hivyo. Inampasa akihisi mwito afanye haraka, ahudhurie na asimame. Inampasa alale mapema ili awe na nguvu na aweke alamu. Ama akikesha basi atapatwa na uvivu huu. Ni wajibu kwake kumcha Allaah na kutekeleza wajibu kwa upande wa mambo yanayomsaidia kuamka. Kwa hiyo asikeshe, bali alale mapema. Akisikia mwito au alamu ikaita aamke na kuswali pamoja na waislamu msikitini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote mwenye kusikia wito kisha asiitikie, basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.” Ibn ´Abbaas akaulizwa: ”Udhuru ni nini?” Akasema: ”Ni khofu au ugonjwa.”
Alijiliwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mtu kipofu akasema:
”Ee Mtume wa Allaah, sina wa kuniongoza kunipeleka msikitini. Je, nina ruhusa ya kuswali nyumbani kwangu?” Akasema: ”Je, unasikia mwito wa swalah?” Akasema: ”Ndio.” Akasema: ”Basi itikia.”
Ikiwa kipofu asiye na wa kumwongoza ameamrishwa kuitikia ambapo anagusa ukuta na kutembea hadi afike msikitini, tusemeje kwa mwenye kuona mwenye uwezo?
Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusudia kuchoma moto nyumba za waliobaki nyuma kwa sababu ya kuacha swalah msikitini.
Kwa hiyo ni wajibu kwa muumini amche Allaah, ajue kuwa Allaah anamuona na aharakie kwenye misikiti usiku na mchana na aswali pamoja na watu. Asipuuze kwa kuswali nyumbani; isipokuwa akiwa mgonjwa. Tunamuomba Allaah atupe uongofu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29421/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%B3%D9%85%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B0%D8%A7%D9%86-%D9%84%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9%C2%A0%D8%AB%D9%85-%D8%BA%D9%84%D8%A8%D9%87-%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%88%D9%85
- Imechapishwa: 14/08/2025
Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mwenye kusikia adhaana naye yuko usingizini, akajaribu kusimama kwa ajili ya swalah lakini usingizi na uvivu vikamshinda. Baada ya watu kumaliza kuswali akasimama na kuswali nyumbani kwake peke yake?
Jibu: Haya ni maovu. Haijuzu kwake kufanya hivyo. Inampasa akihisi mwito afanye haraka, ahudhurie na asimame. Inampasa alale mapema ili awe na nguvu na aweke alamu. Ama akikesha basi atapatwa na uvivu huu. Ni wajibu kwake kumcha Allaah na kutekeleza wajibu kwa upande wa mambo yanayomsaidia kuamka. Kwa hiyo asikeshe, bali alale mapema. Akisikia mwito au alamu ikaita aamke na kuswali pamoja na waislamu msikitini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote mwenye kusikia wito kisha asiitikie, basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.” Ibn ´Abbaas akaulizwa: ”Udhuru ni nini?” Akasema: ”Ni khofu au ugonjwa.”
Alijiliwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mtu kipofu akasema:
”Ee Mtume wa Allaah, sina wa kuniongoza kunipeleka msikitini. Je, nina ruhusa ya kuswali nyumbani kwangu?” Akasema: ”Je, unasikia mwito wa swalah?” Akasema: ”Ndio.” Akasema: ”Basi itikia.”
Ikiwa kipofu asiye na wa kumwongoza ameamrishwa kuitikia ambapo anagusa ukuta na kutembea hadi afike msikitini, tusemeje kwa mwenye kuona mwenye uwezo?
Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusudia kuchoma moto nyumba za waliobaki nyuma kwa sababu ya kuacha swalah msikitini.
Kwa hiyo ni wajibu kwa muumini amche Allaah, ajue kuwa Allaah anamuona na aharakie kwenye misikiti usiku na mchana na aswali pamoja na watu. Asipuuze kwa kuswali nyumbani; isipokuwa akiwa mgonjwa. Tunamuomba Allaah atupe uongofu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29421/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%B3%D9%85%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B0%D8%A7%D9%86-%D9%84%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9%C2%A0%D8%AB%D9%85-%D8%BA%D9%84%D8%A8%D9%87-%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%88%D9%85
Imechapishwa: 14/08/2025
https://firqatunnajia.com/anasikia-adhaana-lakini-anaendelea-kulala/