Swali: Katika hali ya kuswali Haram, lipi lililo bora: kuangalia Ka´bah au mahali pa kusujudia?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah katikaswalah zote na katika kila mahali ni kuangalia mahali pa kusujudia, kwa sababu hilo humfanya mja awe na unyenyekevu zaidi na hukusanya moyo wake zaidi. Isipokuwa katika hali ya Tashahhud, kwani Sunnah ni kuangalia mahali pa kuashiria kidole.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/245)
  • Imechapishwa: 04/03/2026