Amevunja uchumba wa msichana na ameamua kumuoa mama yake

Swali: Nimemchumbia msichana kisha nikavunja uchumba, halafu nikamuoa mama yake. Je, kwa mtazamo wa Shari´ah hili ni halali au haramu?

Jibu: Ikiwa alimchumbia mwanamke kisha akaacha uchumba kabla ya kufunga ndoa, halafu akamuoa mama yake, hakuna tatizo. Ama ikiwa alishafunga ndoa na msichana, basi mama yake anakuwa haramu kwake. Lakini ikiwa hakukuwa na kufunga ndoa, bali ilikuwa ni uchumba tu, kisha akaacha na akamuoa mama yake, hakuna tatizo katika hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1793/حكم-الزواج-بام-من-فسخت-خطوبتها
  • Imechapishwa: 19/12/2025