Ameshindwa kutimiza nadhiri ya kufunga siku 10 kila mwaka

Swali 641: Vipi kuhusu mtu aliyeweka nadhiri ya kufunga kila mwaka siku kumi, lakini akashindwa?

Jibu: Atalipa kafara ya kiapo, kama alivyosema Ibn ´Abbaas. Hakuna anayejulikana kwamba amempinga. Kuna maoni mengine yanayosema kuwa atatoa chakula kwa maskini mmoja kwa kila siku.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 225
  • Imechapishwa: 18/06/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´