Amesamehe deni la mtoto wake katika maradhi aliyokufa kwayo

Swali: Baba yangu aliniazima kiwango fulani cha pesa ili niongeze mke wa pili. Nikamwahidi kumrudishia lakini hata hivyo sikujaaliwa kufanya hivo. Baada ya kuzorota afya ya baba yangu akasema kuwa anamsamehe kila ambaye ana haki juu yake, nikiwemo mimi pia. Lakini ndugu zangu wamepinga na wamesema kuwa hawanisamehe. Je, msamaha wa baba yangu umepita na hauendi kinyume na Shari´ah?

Jibu: Akiwa alisema hivo katika maradhi ambayo alikufa kwayo, hana haki ya kufanya hivo. Ama kama alisema hivo katika maradhi ya kawaida na yenye kuondoka, ana haki ya kufanya hivo. Ama maradhi ya kufa hapa hakuna msamaha, katika hali kama hii mtu huyu anapokonywa haki moja kwa moja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (96) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahthat-12021440h.mp3
  • Imechapishwa: 08/06/2019