Amesahau kupangusa kichwa wakati wa kutawadha

Swali: Wakati wa wudhuu´ nilisahau kupangusa kichwa changu na nikaosha miguu. Je, ni lazima nirudie wudhuu´ wote au nipake kichwa kisha nioshe miguu tena?

Jibu: Unapaswa kupaka kichwa chako na masikio yako, kisha urudie kuosha miguu ikiwa umekumbuka kabla ya kupita muda mrefu. Ikiwa muda umekuwa mrefu, basi unapaswa kurudia wudhuu´ kuanzia mwanzo, kwa sababu kufuatisha viungo bila kukatiza ni faradhi miongoni mwa faradhi za wudhuu´.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/103)
  • Imechapishwa: 19/02/2026