Amesahau al-Faatihah katika Rak´ah ya pili

Swali: Nilisahau kusoma al-Faatihah katika Rak´ah ya pili katika swalah ya ´Aswr. Ni kipi cha wajibu juu yangu?

Jibu: Swali Rak´ah nyingine badala yake. Umeacha nguzo yake. Unatakiwa kuswali Rak´ah nyingine baada ya salamu. Ikiwa hukumbuka isipokuwa baada ya kupita muda basi unatakiwa kuirudi swalah nzima. Kwa sababu haikusihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (14) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-03-11-1434.mp3
  • Imechapishwa: 22/06/2019