Swali: Baadhi ya ndugu wanasema kwamba wao daima huwaambia na kuwakariria watoto waswali. Wakati fulani walimpiga sana mpaka baadhi ya watu wakambeba wakampeleka nyumbani akiwa mgonjwa, kwa sababu ya ulinganizi wake kwa watoto wanaocheza mpira mtaani.
Jibu: Kwa hali yoyote, yeye ana malipo na thawabu kubwa. Hata kama amepigwa, baadhi ya Manabii waliuawa, si kupigwa tu. Baadhi ya Manabii waliuawa bila haki, kama alivyosema Allaah (Ta´ala):
وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ
”… na wakaua Manabii pasi na haki na wakaua wale wanaoamrisha haki katika watu.”[1]
Hivyo ana mtangulizi mwema katika Manabii na watu wema. Lakini inampasa kuwashtaki kwa wenye mamlaka na kwa wakuu wa idara husika ili waadhibiwe. Asinyamaze, kwa sababu wakikuthubutu wewe basi watawathubutu wengine. Ni lazima kutoa taarifa kwa wenye mamlaka katika jambo hili. Akitaka anipigie au aniandikie mimi, kwa idhini ya Allaah nitafanya la lazima katika hilo. Akienda katika idara husika, basi wao hawatapuuza jambo hili. Hili ni jambo kubwa, halifai kunyamaziwa.
Swali: Akikwenda kwa idara ya kuamrisha mema. Je, hawatamsaidia?
Jibu: Ndio; watamsaidia. Aandikie idara hiyo, amwandikie kiongozi Salman, waziri wa mambo ya ndani au naibu wake. Wote hawa – kwa idhini ya Allaah – watatekeleza la lazima. Lakini asilegeze, afuatilie jambo hili, si kwa ajili ya nafsi yake tu, bali ili wasije wakawadhuru wengine. Yeye ana malipo kwa idhini ya Allaah wala hilo halitomdhuru.
[1] 03:21
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1038/توجيه-لمن-تعرض-للضرب-بسبب-امره-بالمعروف
- Imechapishwa: 20/01/2026
Swali: Baadhi ya ndugu wanasema kwamba wao daima huwaambia na kuwakariria watoto waswali. Wakati fulani walimpiga sana mpaka baadhi ya watu wakambeba wakampeleka nyumbani akiwa mgonjwa, kwa sababu ya ulinganizi wake kwa watoto wanaocheza mpira mtaani.
Jibu: Kwa hali yoyote, yeye ana malipo na thawabu kubwa. Hata kama amepigwa, baadhi ya Manabii waliuawa, si kupigwa tu. Baadhi ya Manabii waliuawa bila haki, kama alivyosema Allaah (Ta´ala):
وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ
”… na wakaua Manabii pasi na haki na wakaua wale wanaoamrisha haki katika watu.”[1]
Hivyo ana mtangulizi mwema katika Manabii na watu wema. Lakini inampasa kuwashtaki kwa wenye mamlaka na kwa wakuu wa idara husika ili waadhibiwe. Asinyamaze, kwa sababu wakikuthubutu wewe basi watawathubutu wengine. Ni lazima kutoa taarifa kwa wenye mamlaka katika jambo hili. Akitaka anipigie au aniandikie mimi, kwa idhini ya Allaah nitafanya la lazima katika hilo. Akienda katika idara husika, basi wao hawatapuuza jambo hili. Hili ni jambo kubwa, halifai kunyamaziwa.
Swali: Akikwenda kwa idara ya kuamrisha mema. Je, hawatamsaidia?
Jibu: Ndio; watamsaidia. Aandikie idara hiyo, amwandikie kiongozi Salman, waziri wa mambo ya ndani au naibu wake. Wote hawa – kwa idhini ya Allaah – watatekeleza la lazima. Lakini asilegeze, afuatilie jambo hili, si kwa ajili ya nafsi yake tu, bali ili wasije wakawadhuru wengine. Yeye ana malipo kwa idhini ya Allaah wala hilo halitomdhuru.
[1] 03:21
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1038/توجيه-لمن-تعرض-للضرب-بسبب-امره-بالمعروف
Imechapishwa: 20/01/2026
https://firqatunnajia.com/amepigwa-na-vijana-baada-ya-kuwahimiza-swalah/