Swali: Je, atapaswa mwanamke kulipa swalah wakati wa kusafika endapo alipata hedhi baada ya kuingia muda wa swalah?
Jibu: Kuna tofauti ya maoni kati ya wanazuoni. Baadhi wamesema kuwa anatakiwa kuilipa swalah hiyo na wengine wamesema hapaswi kuilipa. Wengine wamesema ikiwa alichelewesha muda wa swalah hadi ukawa mdogo, basi amefanya uzembe na hivyo analazimika ailipe. Lakini ikiwa hedhi ilimjia katikati ya muda wa swalah au mwanzoni mwa muda bila yeye kuwa amefanya uzembe, basi maoni yaliyo karibu zaidi ni kwamba hailazimiki kuilipa, isipokuwa tu kama alichelewesha kwa kuzembea.
Lakini ikiwa ametwaharika ndani ya muda wa swalah, basi katika hali hii lazima aswali swalah ya wakati huo pamoja na swalah ya kabla yake. Kwa mfano ikiwa ametwaharika wakati wa ´Aswr, ataswali Dhuhr na ´Aswr kwa pamoja. Akisafika wakati wa ´Ishaa, ataswali Maghrib na ´Ishaa zote kwa pamoja. Ibn ’Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa), ’Abdur-Rahmaan bin ’Awf (Radhiya Allaahu ´anh) na kundi la wanazuoni wametoa fatwa hiyo, kwa sababu kwa mwenye udhuru swalah mbili hizi huwa kama muda mmoja.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1191/حكم-من-حاضت-بعد-دخول-وقت-الصلاة
- Imechapishwa: 07/02/2026
Swali: Je, atapaswa mwanamke kulipa swalah wakati wa kusafika endapo alipata hedhi baada ya kuingia muda wa swalah?
Jibu: Kuna tofauti ya maoni kati ya wanazuoni. Baadhi wamesema kuwa anatakiwa kuilipa swalah hiyo na wengine wamesema hapaswi kuilipa. Wengine wamesema ikiwa alichelewesha muda wa swalah hadi ukawa mdogo, basi amefanya uzembe na hivyo analazimika ailipe. Lakini ikiwa hedhi ilimjia katikati ya muda wa swalah au mwanzoni mwa muda bila yeye kuwa amefanya uzembe, basi maoni yaliyo karibu zaidi ni kwamba hailazimiki kuilipa, isipokuwa tu kama alichelewesha kwa kuzembea.
Lakini ikiwa ametwaharika ndani ya muda wa swalah, basi katika hali hii lazima aswali swalah ya wakati huo pamoja na swalah ya kabla yake. Kwa mfano ikiwa ametwaharika wakati wa ´Aswr, ataswali Dhuhr na ´Aswr kwa pamoja. Akisafika wakati wa ´Ishaa, ataswali Maghrib na ´Ishaa zote kwa pamoja. Ibn ’Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa), ’Abdur-Rahmaan bin ’Awf (Radhiya Allaahu ´anh) na kundi la wanazuoni wametoa fatwa hiyo, kwa sababu kwa mwenye udhuru swalah mbili hizi huwa kama muda mmoja.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1191/حكم-من-حاضت-بعد-دخول-وقت-الصلاة
Imechapishwa: 07/02/2026
https://firqatunnajia.com/amepata-hedhi-baada-ya-kuingia-wakati-wa-swalah/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket