Amemwingilia mkewe mchana wa Ramadhaan baada ya matangazo ya redio

Swali: Katika mwezi wa Ramadhaan redio ilitangaza kuwa Ramadhaan inaanza siku ya ijumaa na mimi nikategemea hilo kwa sababu ya kuonekena kutokuwa wazi. Siku ya alkhamisi siku moja kabla ya kuanza kufunga nikamwingilia mke wangu. Baada ya kufunga mwezi huu mtukufu ndipo tukapata kujua kuwa tunalazimika kufunga siku moja kwa sababu tumefunga mwezi mpungufu. Je, nawajibika kutoa kafara juu ya siku hiyo au ni lipi lililo la wajibu kwangu kufanya?

Jibu: Mambo yakiwa kama ulivotaja basi hulazimiki kutoa kafara na wala huna dhambi. Lakini wewe na mke wako nyote wawili mnatakiwa kulipa siku hiyo ambayo mlipata kujua nyuma ya kwamba ilikuwa Ramadhaan.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/315)
  • Imechapishwa: 17/06/2017