Amekata kucha na kunyoa nywele baada ya kutawadha

Swali: Ni ipi hukumu ya kuosha baadhi ya viungo kwa sabuni baada ya kutawadha, pamoja na kunyoa nywele na kukata kucha baada ya wudhuu´?

Jibu: Ikiwa mtu ametawadha, kisha akaosha baadhi ya viungo vyake kwa sabuni, akanyoa nywele zake au akakata kucha zake, basi wudhuu´ wake hauharibiki kwa kufanya hivyo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/284)
  • Imechapishwa: 12/11/2026