Swali: Niliswali nikiongozwa na imamu na nikajiunga naye katika Takbiyrat-ul-Ihraam. Nilisikia kisomo cha al-Faatihah kisha ghafla sauti ya imamu ikakatika na sikusikia Takbiyr ya Rukuu´ kwa sababu ya tatizo lililokuwepo kwenye kipaza sauti. Matokeo yake sikuweza kumfuata imamu na nikawa nimekamilisha swalah yangu kivyangu. Je, swalah yangu ni sahihi kwa kwenda kinyume na imamu?
Jibu: Ndio, swalah yako ni sahihi. Sauti ya imamu ikikatika na mtu akapwekeka kutokamana na imamu swalah yake ni sahihi. Ni mwenye kupewa udhuru. Lakini ikiwa tutakadiria kuwa hili limetokea katika swalah ya ijumaa ambapo sauti ikakatika katika ile Rak´ah ya kwanza na mtu akajitenga na imamu, katika hali hii asiswali swalah ya ijumaa. Kwa sababu amewahi Rak´ah moja peke yake. Endapo sauti itakatika katika Rak´ah ya pili na akajitenga na imamu atatakiwa kukamilisha swalah ya ijumaa kwa sababu amewahi Rak´ah kamilifu. Lakini pindi sauti ya imamu inapokatika mswaliji hatakiwi – ni mamoja mswaliji huyo ni mwanaume au mwanamke – kunuia kuswali kivyake papohapo, anachotakiwa ni yeye kusubiri kwa sababu kuna wakati sauti kweli inakatika lakini wanatengeneza. Akikata tamaa kabisa hapo ndipo anatakiwa kujitenga.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (59) http://binothaimeen.net/content/1349
- Imechapishwa: 21/06/2019
Swali: Niliswali nikiongozwa na imamu na nikajiunga naye katika Takbiyrat-ul-Ihraam. Nilisikia kisomo cha al-Faatihah kisha ghafla sauti ya imamu ikakatika na sikusikia Takbiyr ya Rukuu´ kwa sababu ya tatizo lililokuwepo kwenye kipaza sauti. Matokeo yake sikuweza kumfuata imamu na nikawa nimekamilisha swalah yangu kivyangu. Je, swalah yangu ni sahihi kwa kwenda kinyume na imamu?
Jibu: Ndio, swalah yako ni sahihi. Sauti ya imamu ikikatika na mtu akapwekeka kutokamana na imamu swalah yake ni sahihi. Ni mwenye kupewa udhuru. Lakini ikiwa tutakadiria kuwa hili limetokea katika swalah ya ijumaa ambapo sauti ikakatika katika ile Rak´ah ya kwanza na mtu akajitenga na imamu, katika hali hii asiswali swalah ya ijumaa. Kwa sababu amewahi Rak´ah moja peke yake. Endapo sauti itakatika katika Rak´ah ya pili na akajitenga na imamu atatakiwa kukamilisha swalah ya ijumaa kwa sababu amewahi Rak´ah kamilifu. Lakini pindi sauti ya imamu inapokatika mswaliji hatakiwi – ni mamoja mswaliji huyo ni mwanaume au mwanamke – kunuia kuswali kivyake papohapo, anachotakiwa ni yeye kusubiri kwa sababu kuna wakati sauti kweli inakatika lakini wanatengeneza. Akikata tamaa kabisa hapo ndipo anatakiwa kujitenga.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (59) http://binothaimeen.net/content/1349
Imechapishwa: 21/06/2019
https://firqatunnajia.com/amejitenga-na-imamu-kwa-sababu-ya-kukatika-sauti/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)