Ameinuka kutoka kwenye Rukuu´ kabla ya imamu kimakosa

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusikia sauti ilihali amerukuu pamoja na imamu na akainuka kabla ya imamu kuinuka kwa kudhani kwamba imamu amekwishainuka kutoka kwenye Rukuu´ halafu baada ya hapo imamu akainuka kutoka kwenye Rukuu´ ilihali yeye tayari amekwishasimama?

Jibu: Hili ni jambo la kupewa udhuru. Anatakiwa kurudi na kufanya matendo yake [ya Rukuu´] kabla ya imamu kuinuka. Akidhani kuwa imamu amekwishainuka basi anatakiwa kurudi katika Sujuud kisha amfuate imamu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191047#191047
  • Imechapishwa: 03/09/2018