379 – Mwanamke amefanya ´Umrah kwa kukusudia akiwa na hedhi na hakumwambia mumewe kwa sababu ya kuona aibu. Baadaye akarudi Riyaadh. Afanye nini?

Jibu: Tunamuomba Allaah usalama. Ni lazima arejee na akamilishe ´Umrah yake.

380 – Je, amekwishaolewa na ameingiliwa?

Jibu: Akamilishe ´Umrah hii batili, kisha aingie kwenye Ihraam upya, aikamilishe na achinje kondoo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 133
  • Imechapishwa: 16/08/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´