Ameapa kuwa mke ameachika akitoka nje ya nyumba kisha baadaye akatoka

Swali: Mimi ni mwanaume niliyeoa ambaye nina mtoto mmoja na mke wangu ni mjamzito mwezi wa kwanza. Mke wangu alitoka na ndugu yangu kwenda hospitali bila idhini yangu wala ya baba yangu. Nikakasirika, lakini si hasira ya kupoteza akili. Nikamwapiza mke wangu kwa talaka kwa nia ya kumtisha, si kumtaliki… kisha baada ya siku mbili akatoka na baba yangu kwenda hospitali bila idhini yangu na anasema hakusikia kiapo. Sasa nataka kumrudisha kwa ajili ya mtoto na ujauzito. Ni ipi hukumu? Je, eda yake inaisha lini ikiwa ni mjamzito? Je, ninawajibika kumpa matumizi akiwa kwa wazazi wake?

Jibu: Ikiwa hali ni kama ilivyotajwa, basi maneno haya hukumu yake ni kama kiapo. Kwa sababu kusudio ni kumtisha na kumzuia, si kumtaliki. Kwa hiyo kama ulivyofanya mara ya kwanza; ni juu yako kafara ya kiapo, ambayo ni kulisha masikini kumi au kuwavisha nguo, ikiwa alitoka kwa makusudi na huku anajua. Ama ikiwa hakusikia maneno hayo, basi hakuna juu yako chochote. Kwa sababu ni mjinga au alisahau. Hukumu ni hiyohiyo ikiwa alifanya kwa kusahau. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

Imesihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah amesema: “Nimefanya hivyo.”

Kwa hiyo ikiwa alitoka akiwa hajui, hakusikia kiapo au alisahau, basi hakuna kafara juu yako. Ama ikiwa alikusudia huku anakumbuka, basi unalazimika kutoa kafara ya kiapo kwa kuwa kusudio lako lilikuwa ni kumtisha na kumzuia, si kumtaliki.

[1] 02:286

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3517/حكم-من-حلف-على-زوجته-بالطلاق-بقصد-التهديد-لا-الفراق
  • Imechapishwa: 11/11/2026