Swali: Mimi ninafanya kazi ambayo wengi wao ni manaswara. Katika kazi hiyo kuna takriban wanaume 300 manaswara. Niko katika mawasiliano nao. Nataka kuwalingania Uislamu, lakini sijui lugha yao. Naomba mnipatie vitabu vya kingereza ili niwape?
Jibu: Kuomba vitabu si hapa. Kuomba vitabu hufanywa katika sehemu yake kama ”Daar-ul-Iftaa´” au katika mahali pa kazi. Hakuna ubaya kupewa vitabu kwa ajili ya watu hawa. Huenda Allaah akawaongoza kwa sababu hiyo kwa lugha yao.
Lakini anayefanya kazi pamoja nao, anatakiwa ajihadhari asiwafanye marafiki wa karibu, maswahiba wa ndani na mfano wa hayo. Bali awalinganie kwa Allaah na awahimize kheri, hili ni jambo linalotakiwa. Huenda Allaah akawaongoza kupitia hilo au baadhi yao. Mmeisikia maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh):
“Allaah akimwongoza mtu mmoja kupitia wewe ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote mwenye kuelekeza kwenye kheri, basi atapata mfano wa ujira wa anayeifanya.”
Kwa hiyo mwenye kujaribiwa kuwa pamoja na hawa, ni mamoja iwe ni manaswara, wasiokuwa manaswara, wabudhi au wengineo, basi ajitahidi kuwalingania kwa Allaah. Awe katika Uislamu wake ni mfano mwema ikiwa ni pamoja na kuhifadhi swalah, mkweli katika mazungumzo, kwa kutekeleza amana, kwa kuwapa nasaha waislamu na kwa kujiepusha na udanganyifu na khiyana na mfano wa hayo katika tabia njema za Kiislamu. Afanye hivo ili awe ni kigezo kizuri ili maadui wa Allaah wakimuona na kuona tabia zake njema na sifa zake nzuri, basi hilo liwe sababu ya kuwalingania kwa vitendo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3525/حكم-العمل-مع-النصارى-وكيفية-دعوتهم-الى-الاسلام
- Imechapishwa: 11/11/2026
Swali: Mimi ninafanya kazi ambayo wengi wao ni manaswara. Katika kazi hiyo kuna takriban wanaume 300 manaswara. Niko katika mawasiliano nao. Nataka kuwalingania Uislamu, lakini sijui lugha yao. Naomba mnipatie vitabu vya kingereza ili niwape?
Jibu: Kuomba vitabu si hapa. Kuomba vitabu hufanywa katika sehemu yake kama ”Daar-ul-Iftaa´” au katika mahali pa kazi. Hakuna ubaya kupewa vitabu kwa ajili ya watu hawa. Huenda Allaah akawaongoza kwa sababu hiyo kwa lugha yao.
Lakini anayefanya kazi pamoja nao, anatakiwa ajihadhari asiwafanye marafiki wa karibu, maswahiba wa ndani na mfano wa hayo. Bali awalinganie kwa Allaah na awahimize kheri, hili ni jambo linalotakiwa. Huenda Allaah akawaongoza kupitia hilo au baadhi yao. Mmeisikia maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh):
“Allaah akimwongoza mtu mmoja kupitia wewe ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote mwenye kuelekeza kwenye kheri, basi atapata mfano wa ujira wa anayeifanya.”
Kwa hiyo mwenye kujaribiwa kuwa pamoja na hawa, ni mamoja iwe ni manaswara, wasiokuwa manaswara, wabudhi au wengineo, basi ajitahidi kuwalingania kwa Allaah. Awe katika Uislamu wake ni mfano mwema ikiwa ni pamoja na kuhifadhi swalah, mkweli katika mazungumzo, kwa kutekeleza amana, kwa kuwapa nasaha waislamu na kwa kujiepusha na udanganyifu na khiyana na mfano wa hayo katika tabia njema za Kiislamu. Afanye hivo ili awe ni kigezo kizuri ili maadui wa Allaah wakimuona na kuona tabia zake njema na sifa zake nzuri, basi hilo liwe sababu ya kuwalingania kwa vitendo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3525/حكم-العمل-مع-النصارى-وكيفية-دعوتهم-الى-الاسلام
Imechapishwa: 11/11/2026
https://firqatunnajia.com/wajibu-wako-unapofanya-kazi-na-wasio-waislamu/