Kucheza mpira na kaptula au wakati wa swalah

Swali: Kuna vijana wengi wanaocheza mchezo wa mpira wa miguu katika vilabu na mitaani. Lakini hawafuniki viungo vyao visivyotakiwa kuonekana wakati wa kucheza. Tunaomba neno la kuwaelekeza vijana hawa ili kufunika nyuchi zao na washikamane na Shari´ah ya Kiislamu?

Jibu: Ni wajibu juu ya vijana na wasiokuwa vijana kufunika viungo vyao visivyotakiwa kuonekana na kujihadhari na kuvionyesha, si katika mpira wala katika jambo lingine.

Uchi kwa upande wa mwanaume ni kati ya kitovu na goti. Mwili wote wa mwanamke ni uchi mbele ya mwanaume asiye Mahram. Ama baina ya wanawake ni kama mwanaume; yaliyo juu ya kitovu na chini ya goti si katika uchi kwa mwanamke mbele ya mwanamke. Kwa hiyo wajibu juu ya wanaume na wanawake ni kufunika uchi. Haifai kwake kucheza mpira huku paja lake liko wazi au akiwa na nguo nyepesi. Bali ni lazima kufunika paja lote na yaliyo chini ya kitovu. Ikiwa nguo ni ndefu hadi kufunika chini ya goti, hilo ni kamili na salama zaidi. Inapaswa, bali ni wajibu, kutilia umuhimu jambo hili. Na pia mchezo usiwe wakati wa swalah. Bali uwe katika wakati ambao hakuna swalah ili asipoteze swalah kwa kucheza mpira au jambo lingine. Ikiwa mchezo unasababisha kuacha swalah au kuonyesha uchi, basi unakuwa haramu. Kwa hiyo ni lazima nyakati za mchezo ziwe katika nyakati salama, mbali na swalah. Kila mchezo unaopelekea kuacha swalah au kufanya yale aliyoyaharamisha Allaah, basi unakuwa haramu kwa sababu hiyo. Tunamuomba Allaah atulinde.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3496/وجوب-ستر-العورة-اثناء-اللعب-بكرة-القدم
  • Imechapishwa: 11/11/2026