Ambaye umekataliwa ushahidi wake wa kuona mwezi mwandamo

Swali: Mwanaume alikwenda kwa Qaadhiy kuthibitisha kuona mwezi mwandamo lakini hakukubali uadilifu wake. Je, inamlazimu mwanaume huyu kufunga?

Jibu: Asifunge isipokuwa pamoja na watu, kama alivyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Funga siku ambayo mnawafunga.”

Ikiwa watu watafunga, basi afunge pamoja nao.

Swali: Lakini ameona mwezi mwandamo?

Jibu: Haijalishi kitu, maadamu ushahidi wake umekataliwa basi asifunge wala kufungua isipokuwa pamoja na watu. Haya ndio maoni yenye nguvu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25435/هل-يصوم-من-راى-الهلال-ولو-ردت-شهادته
  • Imechapishwa: 20/03/2025