Ambaye amejiunga na imamu katika Rak´ah ya mwisho

Swali: Ikiwa umefika katika Rak´ah ya mwisho na kupata Rak´ah na Tashahhud pamoja na imamu na mimi niko katika swalah ya Maghrib, kisha nikafika katika Rak´ah ya pili na nikafika katika sehemu ya Tashahhud?

Jibu: Unakaa baada ya Rak´ah ya pili na baada ya Tashahhud wa kwanza, kisha unasimama na kuswali Rak´ah ya tatu kwa kusoma al-Faatihah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1223/حكم-من-ادرك-الامام-في-الركعة-الاخيرة
  • Imechapishwa: 08/02/2026