Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kuadhibu

Swali: Tutawezaje kuoanisha baina ya maneno ya Allaah:

 فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

”Hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

na:

إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ

”Hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.”[2]?

Jibu: Hakuna mgongano baina ya Aayah hizi mbili. Yeye ni mkali wa kuadhibu kwa yule anayeenda kinyume na amri Zake, akavuka mipaka Yake, akajifanya hajali na hakutubu. Sambamba na hilo ni Mwingi wa kusamehe na Mwenye kurehemu kwa yule anayerejea Kwake, akatubia na akaacha madhambi yake. Kwa hivyo mwenye kutubia na kuacha madhambi hupata msamaha na rehema, na mwenye kushikilia kufanya maasi na akajifanya hajali anastahiki adhabu, isipokuwa Allaah akimsamehe (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] 02:226

[2] 59:7

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30919/ما-كيفية-الجمع-بين-ايات-المغفرة-وشدة-العقاب
  • Imechapishwa: 15/09/2025