Swali: Je, Allaah anasifiwa kufanya vitimbi?

Jibu: Katika kulipiza vitimbi. Ni kama ambavo alivyojisifu Mwenyewe:

وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ

“Na wanapanga vitimbi na Allaah anapanga vitimbi; na Allaah ni mbora wa wenye kupanga vitimbi.”[1]

Katika kulipiza dhuluma za wenye kufanya njama. Ni vitimbi vya haki na sio vitimbi vya mchezo. Ni ufanyaji wa vitimbi wa haki, istihzai ya haki na hadaa ya haki.

Swali: Je, hiyo ni kwa njia ya kulipiza kisasi?

Jibu: Ndio, malipizi.

Swali: Vipi kuhusu kupindisha maana ya sifa hii?

Jibu: Ni kosa kupindisha maana yake. Lakini ni sawa kuelezea athari yake kwa ambapo Analipiza na kumuadhibu ambaye anafanya njama, akadhaa na kucheza shere. Hiyo ni athari yake. Miongoni mwa mambo inayopelekea ni adhabu. Ni kama ambavo Anaghadhibika. Miongoni mwa mambo yanayopelekea ni kumuadhibu yule anayemghadhibikia. Anaghadhabika na kukasirika (Subhaanah). Miongoni mwa mambo ghadhabu inayopelekea ni kumuadhibu yule aliyemghadhibikia. Miongoni mwa mambo radhi na rehema inayopelekea ni kumtunza yule anayemrehemu na akamridhia.

[1] 08:30

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24626/هل-يوصف-الله-تعالى-بالمكر
  • Imechapishwa: 15/11/2024