al-Waadi´iy kuhusu shaytwaan anavyomtia wasiwasi al-Qaradhwaawiy

Masuala ya mwanamke kutawala anasema kuwa yeye anaona kuwa haina neno [mwanamke] akawa raisi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Hawatofaulu watu wenye kutawaliwa jambo lao na mwanamke.”

al-Qardhwaawiy ni mwanachuoni muovu ambaye Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema juu yake na wengine mfano wake:

“Kikubwa ninachokikhofia katika Ummah wangu ni viongozi wenye kupotosha.”

Ameipokea Abu Daawuud kupitia kwa Thawbaan.

Anasema tena:

“Kikubwa ninachokhofia katika Ummah wangu ni mnafiki hodari wa kuzungumza.”

Mimi nafikiri kuwa shaytwaan ndiye hutia wasiwasi kwenye moyo wa al-Qardhwaawiy akazungumza anavyozungumza. Na bado kutajitokeza mambo mbali mbali kutoka kwa al-Qardhwaawiy.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 9
  • Imechapishwa: 08/10/2016