al-Fawzaan kutumia vidonge vya kuzuia hedhi kwa ajili ya Ramadhaan

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kutumia vidonge vinavyozuia hedhi ili aweze kufunga Ramadhaan bila kusitisha?

Jibu: Hakuna ubaya katika hilo ikiwa vidonge hivyo havimdhuru katika afya yake na vinazuia kutoka kwa damu. Hakuna tatizo kuvitumia. Na maadamu damu haijashuka, basi swawm yake ni sahihi.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/406-407)
  • Imechapishwa: 18/02/2026