Swali: Shaykh Hammaad al-Answaariy (Rahimahu Allaah) ametaja katika kitabu chake “Masaa-il fiyl-´Aqiydah” katika tafsiri ya “al-Faatihah” ya kwamba Tawhiyd ni vigawanyo vine ambapo akataja ya kwamba kigawanyo cha nne ni “Tawhiyd-ul-Mutaaba´ah” bi maana kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Unasemaje juu ya hilo?
Jibu: Ndio, kuna baadhi yao wamesema kuwa kuna kigawanyo cha nne. Lakini uhakika wa mambo sio katika Tawhiyd. Ni katika kufuata, al-Ittibaa´ na kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haisemwi kuwa ni Tawhiyd. Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah kwa ´ibaadah. Je, kunaweza kusemwa ya kwamba mwenye kwenda kinyume na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakuwa mshirikina? Mwenye kwenda kinyume na Tawhiyd anakuwa mshirikina tofauti na mwenye kwenda kinyume na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtu huyu anakuwa ni mtenda dhambi. Shaykh Hammaad amefuata maoni ya baadhi yao [wanachuoni]. Lakini hata hivyo yanahitajia kuangaliwa vizuri.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (36) http://alfawzan.af.org.sa/node/2133
- Imechapishwa: 13/07/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket