Swali: Ni ipi kauli yenye nguvu juu ya Luqmaan; ni Nabii au mtu mwenye hekima miongoni mwa wenye hekima?

Jibu: Ni nani aliyesema kuwa ni Luqmaan ni Mtume? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Je, hukusikia kauli ya mja mwema… “

Tofauti iko kwa Khidhr kama ni Nabii au mja mwema. Kuhusu Luqmaan hakuna yeyote aliyesema kuwa ni Nabii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (36) http://alfawzan.af.org.sa/node/2133
  • Imechapishwa: 13/07/2020