al-Baqarah nyumba ya kwenye rekodi

Swali: Baadhi ya watu wanaweka rekodi ya Suurah al-Baqarah na wanaikariri nyumbani kwa kuchelea majini au mfano wake. Ni upi usahihi wa hilo?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika shaytwaan hukimbia kutoka katika nyumba ambayo kunasomwa ndani yake Suurah al-Baqarah.”

Lakini kisomo hichi kinatakiwa kiwe kutoka kwa mtu mwenyewe. Lakini ukiweka rekodi si kisomo kutoka kwa mtu. Kisomo kinatakiwa kiwe chneye kutoka kwa mtu. Hivi ndio bora na kamilifu zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-26-12-1435هـ
  • Imechapishwa: 19/06/2022