Swali: Nimesikia maneno ya mmoja wa wanazuoni Saudi Arabia, anayejulikana kwa kheri, akisema kwamba Sunnah ya Allaah itaendelea mpaka siku ya Qiyaamah: pindi ukafiri, ufasiki na maasi vinapozidi na uovu kusambaa, jambo ambalo ni dalili ya kushuka kwa adhabu na maangamizi. Allaah aliangamiza mataifa yaliyopita kwa mafuriko, upepo na mengineyo. Sasa watu wamezidi katika ukafiri na maasi na balaa imeenea duniani kote isipokuwa anavyotaka Allaah. Wakati huu hautakuwa kwa maji wala kwa hewa, bali kwa moto. Hakika Allaah ametakasika na kufanya mambo bure na haikuumbwa atomu au silaha za nyuklia isipokuwa kwa hekima kubwa. Siku moja dunia itatakaswa na watabaki waumini wa kweli. Amesema (Ta´ala):
وَلَا يَزَالُ الَّذِينَ كَفَرُوا تُصِيبُهُم بِمَا صَنَعُوا قَارِعَةٌ أَوْ تَحُلُّ قَرِيبًا مِّن دَارِهِمْ حَتَّىٰ يَأْتِيَ وَعْدُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ
”Wale waliokufuru hawatoachwa kusibiwa na balaa kwa sababu ya yale waliyoyatenda au ikawateremkia karibu na nyumba zao mpaka ifike ahadi ya Allaah; hakika Allaah haendi kinyume na miadi Yake.”[1]
Je, yepi maoni yako yenu kuhusu haya?
Jibu: Bila shaka jambo ni kubwa na hali iliyopo inaashiria khatari, kwa sababu uovu umeenea sana. Hakika yale yaliyopo leo miongoni mwa watu aina za ukafiri, upotofu, maasi ya wazi na uhalifu mwingi, ni dalili ya khatari kubwa na watu wako katika khatari kubwa. Lakini kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kitaendelea kuwepo kundi katika ummah wangu lililo juu ya haki, halitadhuriwa na waliowakosesha nusura wala waliowapinga mpaka itakapokuja amri ya Allaah.”
Kwa hiyo lazima kuwe na kundi litakalobaki miongoni mwa wanazuoni na waumini juu ya uongofu na uadilifu. Hawatadhuriwa na wanaowapinga wala wanaowatosa mpaka amri ya Allaah ifike, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Itakuja zama ambapo Allaah atawaangamiza makafiri wote na hautabaki isipokuwa Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa hilo litatokea kupitia kwa ´Iysaa (´alayhis-Salaam). Atakaposhuka ´Iysaa (´alayhis-Salaam), basi atahukumu kwa Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba ataua nguruwe, atavunja msalaba na ataondoa kodi na kwamba hatakubali isipokuwa Uislamu tu. Katika zama zake, Allaah ataziangamiza dini zote mpaka ubaki Uislamu pekee na ´ibaadah zote ziwe kwa Allaah peke Yake. Ama kabla ya hapo majaribu na mitihani vitaendelea. Allaah huwajaribu watu kwa watu wengine; hawa wanapata adhabu, wengine pia wanapata adhabu na wengine wanaokoka. Huu ndio mwenendo wa Allaah kwa waja Wake. Baadhi ya mataifa yaliangamizwa kwa adhabu ya jumla, kama watu wa Nuuh, na wengine walipewa adhabu maalum, kama watu wa Huud kwa upepo mkali na watu wa Swaalih (ambao ni kina Thamuud) kwa ukelele na mtetemeko wa ardhi na wakati huohuo wengine hawakuangamizwa. Watu wa Luutw waliadhibiwa kwa kupinduliwa miji yao na kufukiwa ardhini kutokana na maovu yao makubwa kama shirki, uovu na uzinzi wa kiume kwa kiume na uhalifu mwingine, kama kuvunja amani njiani. Fir´awn na watu wake waliangamizwa kwa kuzamishwa baharini na huku wana wa israaiyl wakiokolewa. Adhabu zinaweza pia kutokea kwa silaha za kisasa, kama ilivyotokea Japani katika vita vya mwisho na sehemu nyingine ambapo mamilioni ya watu waliangamia. Hata leo, vita vikubwa vinaweza kutokea na kuangamiza mamia ya maelfu au mamilioni ya watu. Tunamuomba Allaah atulinde. Vilevile kuna adhabu nyingine kama ajali za ndege zinazoua mamia ya watu na ajali za magari zinazoua watu wengi. Haya yote ni aina ya adhabu. Tunamuomba Allaah atupe usalama na afya.
[1] 13:31
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3202/اسباب-وقوع-العذاب-والهلاك
- Imechapishwa: 16/11/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3202/اسباب-وقوع-العذاب-والهلاك
Imechapishwa: 16/11/2026
https://firqatunnajia.com/aina-mbalimbali-ya-adhabu-ya-allaah-kwa-waja-kutokana-na-madhambi-wanayoyafanya/