Wudhuu´ wa ambaye hakupangusa kichwa chake chote

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye hakupangusa kichwa chake chote kwa maji wakati wa kutawadha? Je, wudhuu´ wake ni sahihi?

Jibu: Ni wajibu kupangusa kichwa chote wakati wa wudhuu´. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَامْسَحُواْ بِرُؤُوسِكُمْ

“… na panguseni vichwa vyenu… ”[1]

Pia kwa mujibu wa Hadiyth iliyopokelewa na al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa ´Abdullaah bin Zayd bin ´Aaswim (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kuhusu namna ya kutawadha, ambaye amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipangusa kichwa chake ambapo akaanza kupeleka mikono yake kutoka mbele ya kichwa kuelekea nyuma, kisha akairejesha mahali alipoanzia.”

Imekuja katika upokezi mwingine wa al-Bukhaariy na Muslim:

“Alianza sehemu ya mbele ya kichwa chake mpaka akafikisha mikono yake kwenye kisogo, kisha akairejesha mahali alipoanzia.”[2]

[1] 05:06

[2] al-Bukhaariy (186) na Muslim (01/145).

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/211-212)
  • Imechapishwa: 16/11/2026