Muulizaji: Vipi tumnasihi? Vipi tuwanasihi vijana hapa Jordan?

an-Najmiy: Ninawanasihi vijana wasimsikilize na wala wasihudhurie darsa zake.

Muulizaji: Je, kutokana na haya mambo tunaweza kusema kuwa mtu huyu ni wa Bid´ah au mpotofu?

an-Najmiy: Yatosheleza kuwa hivyo kama anamuheshimu na kumsema vizuri Abul-Hasan na al-Maghraawiy.

Muulizaji: Yatosha kuwa mtu wa Bid´ah?

an-Najmiy: Ndio.

Muulizaji: Wallaahi si haya tu Shaykh. Mpaka hivi leo anawatetea. Hasemi kuwa al-Qaradhwaawiy ni mtu wa Bid´ah au mpotofu anawapoteza wengine. Niliongea nae na imesajiliwa. Na nilimwambia hatujawahi kukusikia hata mara moja ukisema kuwa al-Qaradhwaawiy ni mpotofu na ni mtu wa Bid´ah anayepotosha wengine. Anasema mimi siwezi kujumuisha kauli zote hizi na kuzisema katika kikao kimoja, mbali na yote aliosema. Bali anasema kuwa al-Qaradhwaawiy ni mwanachuoni na msomi.

an-Najmiy: Subhaan Allaah! Kwani mtu huyu anafuata Sunnah au kapinda katika Sunnah?

Muulizaji: Wallaahi Shaykh mpaka hivi leo anadai kuwa ni katika wanafunzi wa Shaykh al-Albaaniy. Naweza kukupata jina lake? Anaitwa Mashhuur Hasan al-Salmaan.

an-Najmiy: Ni Mashhuur?

Muulizaji: Ndio.

an-Najmiy: Ni yule anayefanya uhakiki wa vitabu]?

Muulizaji: Anafanya nini?

an-Najmiy: Anafanya uhakiki?

Muulizaji: Ndio, sahihi. Ni mtu anafanya uhakiki.

an-Najmiy: Aha sawa! Hasbuna Allaah wa Ni´imal wakiyl.

Muulizaji: Unajua nini kutoka kwake Shaykh?

an-Najmiy: Mwanzoni nilikuwa sijui kitu. Nilikuwa sijamwangalia au kusikia kitu kutoka kwake.

Muulizaji: Wallaahi Shaykh nilikaa nae karibu mwaka mmoja tukifanya utafiti katika maktabah. Nilipokuja katika masuala haya, nikamuacha.

an-Najmiy: Muache! Vijana wanaokutii waambie wasikae nae.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/jI8YXBxoU54
  • Imechapishwa: 28/07/2020