Umeandika kwenye barua yako:

“Kuna vitabu vinavyojulikana ambavyo ni vibaya zaidi kuliko vitabu vyake. Kuna walinganizi, walio hai maiti, waliopinda zaidi kuliko yeye.”

Himdi zote ni za Allaah ambaye amekufanya kutamka haki pasi na wewe kuhisi hilo. Umekubali mwenyewe kuwa kuna shari kwenye vitabu vyake na upindaji kwenye mfumo wake. Maneno yako yameshabihiana na kujigonga kwa Ahl-ul-Bid´ah. Hivyo basi, kuwa mwangalifu!

Pili ni wajibu kwa wanachuoni kuwabainishia watu haki kwa kadri na uwezo wao.

Tatu mfumo huu umetutia kwenye mitihani katika majumba yetu. Umeharibu akili za wana wetu. Wamekuwa hawamtambui tena baba yake, rafiki yake mwenye kumjali na mwalimu wake mwenye kulea. Hawaamini nasaha za wanasihiaji wala ukosoaji wa wakosoaji ikiwa mtu si kutoka katika kundi lao. Wanafanana na wale ambao Allaah amesema juu yao:

وَلاَ تُؤْمِنُواْ إِلاَّ لِمَن تَبِعَ دِينَكُمْ

“Na wala msimwamini isipokuwa tu yule anayefuata dini yenu!”[1]

Watu hawa walisema:

“Msimwamini yeyote isipokuwa yule ambaye yuko katika pote lenu.”

Hili liliwajibisha matahadharisho juu ya mfumo huu, muasisi wake na matawi yake kama Suruuriyyah na Qutbiyyah. Hili limewajibisha ukhusishaji huu kwa vile mfumo huu umeenea katika mji wetu wote na kuharibu akili za vijana wetu. Imewageuza kuwa wapinduaji Takfiyriyyuun na magaidi. Kwa hivyo haishangazi wanafunzi Salafiyyuun wakikaripia mfumo huu na kuonyesha makosa yake ili kuhakikisha haki na kuwatakia kheri viumbe ili kujikurubisha kwa Allaah (Ta´ala) na kupigana vita katika njia Yake:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا

“Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hakika Sisi hatupotezi malipo ya atendae matendo mema.”[2]

[1] 03:73

[2] 18:30

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Radd-ul-Jawaab, uk. 30
  • Imechapishwa: 05/07/2020