Swali: Je, mtu ataadhini na kukimu kwa kila swalah wakati wa kukusanya swalah?

Jibu: Mtu akikusanya basi ataadhini juu ya ile swalah ya kwanza na kukimu juu ya kila swalah ya faradhi. Isipokuwa ikiwa kama atakuwa ndani ya mji. Katika hali hiyo ile adhaana ya ndani ya mji inatosha na atakimu tu juu ya kila faradhi.  Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) siku ya ´Arafah aliadhini kisha akakimu na kuswali Dhuhr halafu akakimu na kuswali ´Aswr. Vivyo hivyo Muzdalifah kulipoadhiniwa na kukimiwa ambapo akaswali Maghrib kish ndipo akaswali ´Ishaa.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/192)
  • Imechapishwa: 12/06/2026