Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

77 – Aliye na furaha ni yule anayefurahishwa na mipango ya Allaah, aliyekula khasara ni yule asiyefurahishwa na mipango ya Allaah. Makadirio ni siri ya Allaah (Ta´ala) katika viumbe Wake. Hakuna Malaika aliye karibu wala Mtume aliyetumilizwa aliyemfanya kujua jambo hilo.

MAELEZO

Huyu hakula khasara kutokana na makadirio ya Allaah (´Azza wa Jall). Hakika si venginevyo amekula khasara kutokana na matendo yake mwenyewe ambayo Allaah amemkadiria. Yule ambaye Allaah amemkadiria kufurahi au kula khasara, basi atamfanyia wepesi katika hayo.

Makadirio ni siri ya Allaah (Ta´ala) kwa njia ya kwamba mtu hawezi kuifikia vovyote atakavyojaribu kuipekua. Kwa ajili hiyo mtu asiichoshe nafsi yake. Wewe kinachokupasa ni kuamini mipango na makadirio, fanya matendo mema na jiepushe na matendo maovu. Haikuhusu kupekua siri ya makadirio wala hujapewa kazi hiyo. Allaah (´Azza wa Jall) pekee ndiye anayejua hilo. Si Malaika, Mitume wala wengineo wanajua mambo yaliyofichikana. Hata mbora wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ

“… na lau ningekuwa najua ya ghaibu, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri na wala lisingelinigusa ovu.”[1]

[1] 7:188

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 111-112
  • Imechapishwa: 30/10/2024