Swali: Nimesikiliza moja ya kaseti ya Imaam Muhammad Naaswiyrud-Diyn al-Albaaniy katika masuala anaposema imamu “Aamiyn” nanyi semeni “Aamiyn”. Akakazia hilo.

Ibn ´Uthaymiyn: Kasema nini?

Muulizaji: Kasema ni wajibu anaposema imamu “Aamiyn” kusema baada yake “Aamiyn” na kwamba uliyoyasema ni kosa.

Ibn Ibn ´Uthaymiyn: Umemsikia kweli kasema hivyo?

Muulizaji: Ndiyo.

Ibn ´Ithaymiyn: Je, mimi, al-Albaaniy na mwengine yeyote tumelindwa na makosa? Hapana, hatukulindwa. Je Shaykh al-Albaaniy ana makosa mengi au kupatia kwake ndiyo kwingi?

Ibn ´Uthaymiyn: Bila shaka kupatia kwake ndiyo kwingi. Na hili ni moja ya makosa yake. Kwa sababu maneno ya Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaposema imamu “Aamiyn” nanyi semeni “Aamiyn” yanafasiriwa na ile Hadiyth nyingine.”

Anaposema imamu:

وَلاَ الضَّالِّينَ 

“Wala waliopotea.” (01:07)

Semeni “Aamiyn”.” Lini atasema? Atasema hivi pamoja na imamu. Maana ya “Akisema imamu “Aamiyn” yaani akifika mahala anaposema “Aamiyn” au anapoanza kusema “Aamiyn”.

al-Albaaniy mazuri yake ni mengi. Na kupatia kwake ni kwingi kuliko makosa na wala hili halimteremshi kwa kufanya kosa. Lakini ni Mujtahid kama wengine. Akipatia ana ujira mara mbili na akikosea ana ujira mara moja na kosa lake linasamehewa.

Mwanafunzi: Nilisoma katika “Silsilah al-Ahaadiyth as-Swahiyhah”, mjalada wa sita, alirejea baada ya kubainikiwa na akasema mtu anasema “Aamiyn” pamoja na imamu.

Ibn ´Uthaymiyn: Alhamdulillaah. Hii ndiyo haki – Allaa akitaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (200 B) Tarehe: 1419-11-23/1999-03-10
  • Imechapishwa: 27/06/2021