Wanaingia katika haya Suufiyyah ambao wamefanya kuchezacheza, ngoma na nyimbo kuwa ni sehemu katika dini. Wanaita kuwa ni Anaashiyd na Qaswiydah. Wanaziimba na huku wakijikurubisha kwa Allaah. Uhakika wa mambo ni nyimbo na ngoma za haramu. Ni pumbao zilizo za haramu.
Wanaingia vilevile katika haya – nao ni msitari wa kwanza – wale ambao wameegemea katika matamanio na yale yanayopendeza kwenye nafsi zao na wanazipa nafsi zao vile inavyovipenda ijapokuwa vitu hivyo vinaenda kinyume na dalili. Huku ni kuifanya dini kuwa upuuzi na mchezo. Wanaingia ndani yake watenda madhambi ambao hawayajali maamrisho ya dini na wanafuata yale yanayopendwa na nafsi na matamanio yao.
Kadhalika wanaingia Suufiyyah wafanya ´ibaadah ambao wameingiza ndani ya ´ibaadah yasiyokuwemo. Bali wameingiza ndani mambo ya ngoma na kucheza ambayo yanapingana nayo. Wameyafanya haya kuwa ni dini na wanaimba Qaswiydah za nyimbo kama wanavyofanya manaswara wanapoimba nyimbo zao. Yote haya ni katika kuifanya dini kuwa ni pumbao na mchezo.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 197-198
- Imechapishwa: 13/01/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)