45 – Hakika aliyehishimiwa zaidi mbele ya Allaah (Ta´ala) miongoni mwa wachamungu ni yule ambaye ulimi wake haukauki kwa kumtaja Yeye. Kwani amemuogopa katika amri na makatazo Yake na pia ameufanya Dhikr kuwa ni alama yake. Kumcha Allaah kumemsababishia kuingia Peponi na kuokoka na Moto. Haya ndio malipo na ujira. Dhikr inamletea ukaribu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na heshima ya kuwa karibu Naye. Hicho ndio cheo.
Wafanyao kazi kwa ajili ya Aakhirah wako wa aina mbili: miongoni mwao wako wanaofanya kwa ajili ya ujira na thawabu, na miongoni mwao wako wanaofanya kwa ajili ya cheo na daraja. Kwa hiyo wanashindana na wenzao katika kupata nyongeza ya ukaribu kwa Allaah (Ta´ala) na daraja. Allaah (Ta´ala) ameyataja makundi haya mawili pale aliposema:
إِنَّ الْمُصَّدِّقِينَ وَالْمُصَّدِّقَاتِ وَأَقْرَضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعَفُ لَهُمْ وَلَهُمْ أَجْرٌ كَرِيمٌ
”Hakika wanaume watoao swadaqah na wanawake watoao swadaqah na wakamkopesha Allaah mkopo mzuri, watazidishiwa maradufu na watapa ujira mtukufu.”[1]
Hawa ndio watu wa ujira na thawabu. Kisha akasema:
وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصِّدِّيقُونَ
”Wale waliomuamini Allaah na Mtume Wake, hao ndio mashahidi… ”
Hawa ndio watu wa cheo na ukaribu. Kisha akasema:
وَالشُّهَدَاءُ عِندَ رَبِّهِمْ لَهُمْ أَجْرُهُمْ وَنُورُهُمْ
”… hao ndio mashahidi wa kweli mbele ya Mola wao. Watapa ujira wao na nuru yao!”[2]
Imesemwa kuwa huu ni mfuatano wa khabari kuhusu wale waliomwamini Allaah na Mitume Yake ya kwamba wao ni wakweli na kuwa wao ni mashahidi ambao watashuhudia juu ya nyumati. Kisha akaelezea ya kwamba watapata malipo na nuru yao. Kwa hiyo akasimulia juu yao kwamba watapata mambo manne: kuwa wao ni wakweli na mashahidi, jambo ambalo ni daraja na cheo.
Imesemekana vilevile ya kwamba muktadha unaishia kwa maneno Yake (Ta´ala):

Kisha muktadha mpya kuhusu mashahidi huanza katika:

”… hao ndio mashahidi wa kweli mbele ya Mola wao. Watapa ujira wao na nuru yao!”[3]
Katika hali hiyo amewataja wenye kutoa swadaqah, wafanyao wema na ihsani, kisha waumini ambao imani imekita na kujaa ndani ya nyoyo zao. Basi hao ni wakweli, wale wanaojua na kufanya matendo. Wale waliotajwa wa mwanzo ni watu wa wema na ihsani, lakini hawa wa mwisho wana ukweli zaidi mkamilifu zaidi kuliko wa mwanzo.
[1] 57:18
[2] 57:19
[3] 57:19
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 165-167
- Imechapishwa: 08/09/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 165-167
Imechapishwa: 08/09/2025
https://firqatunnajia.com/93-watu-watukufu-zaidi-mbele-ya-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket