Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

73 – Allaah amekwishajua tokea mwanzo idadi ya ambao wataingia Peponi na idadi ya watakaoingia Motoni. Idadi hiyo haitozidi na wala haitopungua.

MAELEZO

Maneno haya yanahusiana na mipango na makadirio. Kuamini mipango na makadirio ni moja katika zile nguzo sita za imani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar, kheri na shari yake.”[1]

Ndani ya Qur-aan Allaah (Jalla wa ´Alaa) anasema:

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ

”Hakika kila kitu Sisi Tumekiumba kwa makadirio.”[2]

وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا

”Ameumba kila kitu kisha akakikadiria kipimo sawasawa.”[3]

Hakuna kitu kinachokuwepo pasi na kukadiriwa. Wala hakuna vitu vinavyotokea kwa bahati mbaya au bila utambuzi wa Allaah. Kila kitu kinachotokea kimekadiriwa, kimeandikwa.

[1] Muslim (8).

[2] 54:49

[3] 25:2

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 105-106
  • Imechapishwa: 29/10/2024