90. Hapo ndipo Mtume alipata mwisho wa al-Baqarah

86 – Abu Dharr al-Ghifaariy amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nimepewa Aayah mbili mwishoni mwa Suurah al-Baqarah kutokea chini ya ´Arshi. Hajapewa nazo Nabii yeyote kabla yangu.”

Wapokezi wake ni wenye kuaminika.

87 – ´Uqbah bin ´Aamir amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kusoma Aayah mbili mwishoni mwa Suurah al-Baqarah… Allaah amenipa nazo kutokea chini ya ´Arshi.”

Cheni ya wapokezi ni njema[1].

[1] Ameipokea Ahmad na wengineo kwa cheni mbili za wapokezi nzuri, kama nilivyobainisha katika “as-Swahiyhah” (1482).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 107-108
  • Imechapishwa: 03/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy