Kulingana juu ni sifa kamilifu na iliyothibiti kuhusiana na Yeye (Subhaanah) ambaye ana ukuu na utukufu. Qur-aan na Sunnah zote zinafahamisha sifa hiyo kwa namna ambayo Mola (Subhaanah) amejithibitishia nayo Mwenyewe ndani ya Kitabu Chake na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) katika Sunnah zake. Isitoshe waislamu wameafikiana juu ya kuthibiti kwake.

Sifa hiyo imetajwa mara nyingi ndani ya Qur-aan na kwa njia mbili: ikiambatana na kihusishi (على) na kuambatana na kiambishi (إلى). Njia ya kwanza, nayo ni kwamba sifa hiyo inaambatana na kihusishi (على), imetajwa mara saba ndani ya Qur-aan. Mola (Subhaanah) anajisifu kwayo na kuifanya kuwa ni miongoni mwa sifa Zake kamilifu na tukufu. Isitoshe Anaiambatanisha na sifa Zake nyingine za kustaajabisha, kamilifu na tukufu, jambo ambalo linajulisha sifa hiyo kumthibitikia Yeye kama zilivyo sifa Zake nyingine. Shaykh na ́Allaamah Muhammad al-Amiyn ash-Shanqwiytwiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tambua ya kwamba Kulingana juu ni sifa kamilifu na tukufu ambayo amejisifu kwayo Mola wa mbingu na ardhi. Kinachoithibitisha hayo ni kwamba Yeye hakuitaja pahali popote ndani ya Kitabu Chake isipokuwa ameimbatanisha na sifa Zake kamilifu na tukufu ambazo ni za kushangaza. Nitakupa mfano wa hilo:

1 – Allaah ametaja Kulingana juu kwa mara ya kwanza katika ”al-A´raaf”. Amesema:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesiupesi na [ameumba] jua na mwezi na nyota vimetiishwa kwa amri Yake. Tanabahi! Ni Vyake pekee uumbaji na amri. Amebarikika Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]

Je, kuna yeyote awezaye kukanusha chochote katika sifa hizi zinazofahamisha ukamilifu na utukufu?

2 – Allaah amesema sehemu ya pili katika ”Yuunus”:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ إِنَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ بِالْقِسْطِ ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ إِنَّ فِي اخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ

”Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ‘Arshi; anaendesha mambo yote. Hakuna mwombezi yeyote isipokuwa baada ya idhini Yake. Huyu ndiye Allaah, Mola Wenu, hivyo basi mwabuduni. Kwa nini hamkumbuki? Kwake ni marejeo yenu nyote; ni Ahadi ya Allaah ya kweli. Hakika Yeye anaanzisha uumbaji kisha anaurudisha ili awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakafanya mema. Na wale waliokufuru watapata kinywaji cha maji ya kuchemka mno na adhabu iumizayo kwa sababu ya kukufuru kwao. Yeye ndiye Aliyefanya jua kuwa ni mwanga na mwezi kuwa ni nuru na akaukadiria vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu. Allaah hakuumba hivyo isipokuwa kwa haki. Anapambanua waziwazi alama kwa watu wanaojua. Hakika katika kutofautiana usiku na mchana na alivyoviumba Allaah katika mbingu na ardhi bila shaka kuna ishara kwa watu wenye kumcha Allaah.”[2]

Je, kuna yeyote awezaye kukanusha chochote katika sifa hizi zinazofahamisha ukamilifu na utukufu?

3 – Amesema (Jalla wa ´Alaa) sehemu ya tatu katika ”ar-Ra´d”:

اللَّـهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُم بِلِقَاءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ وَهُوَ الَّذِي مَدَّ الْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْهَارًا ۖ وَمِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ جَعَلَ فِيهَا زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ ۖ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ وَفِي الْأَرْضِ قِطَعٌ مُّتَجَاوِرَاتٌ وَجَنَّاتٌ مِّنْ أَعْنَابٍ وَزَرْعٌ وَنَخِيلٌ صِنْوَانٌ وَغَيْرُ صِنْوَانٍ يُسْقَىٰ بِمَاءٍ وَاحِدٍ وَنُفَضِّلُ بَعْضَهَا عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الْأُكُلِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

”Allaah ambaye ameinua mbingu bila ya nguzo mnaziona kisha akalingana juu ya ‘Arshi na akavitiisha jua na mwezi – vyote vinakwenda mzunguko hadi muda maalum uliokadiriwa. Anaendesha mambo anapambanua waziwazi Aayah ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mala wenu. Na Yeye ndiye aliyetandaza ardhi na akafanya humo milima imara na mito na kila aina ya mazao amefanya humo jozi mbilimbili; anafunika usiku juu ya mchana. Hakika katika hayo kuna alama kwa watu wanaozingatia. Katika ardhi kuna vipande vyake tofauti vinavyopakana na mabustani ya mizabibu na mazao na mitende inayochipuka katika shina moja na isiyochipuka katika shina moja; vinanyweshezwa kwa maji ya aina moja na tunavifanya baadhi kuwa bora zaidi kuliko vingine katika ladha na lishe. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaotia akilini.”[3]

Je, kuna yeyote awezaye kukanusha chochote katika sifa hizi zinazofahamisha ukamilifu na utukufu?

4 – Amesema sehemu ya nne katika ”Twaa Haa”:

طه مَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لِتَشْقَىٰ إِلَّا تَذْكِرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ تَنزِيلًا مِّمَّنْ خَلَقَ الْأَرْضَ وَالسَّمَاوَاتِ الْعُلَى الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَمَا تَحْتَ الثَّرَىٰ وَإِن تَجْهَرْ بِالْقَوْلِ فَإِنَّهُ يَعْلَمُ السِّرَّ وَأَخْفَى اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ

”Twaa Haa. Hatujakuteremshia Qur-aan ili upate mashaka; isipokuwa ni Ukumbusho kwa anayekhofu. Ni Uteremsho kutoka kwa Yule aliyeumba ardhi na mbingu zilizo juu kabisa. Mwingi wa rehema amelingana juu ya ‘Arshi. Ni Vyake pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini na vilivyomo baina yake na vilivyomo chini ya udongo. Ukiongea kwa sauti ya juu, basi hakika Yeye anajua siri na yanayofichika zaidi ya siri. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye; Anayo majina mazuri kabisa.”[4]

Je, kuna yeyote awezaye kukanusha chochote katika sifa hizi zinazofahamisha ukamilifu na utukufu?

5 – Amesema sehemu ya tano katika ”al-Furqaan”:

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحْ بِحَمْدِهِ ۚ وَكَفَىٰ بِهِ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا

”Mtegemee Aliye hai ambaye hafi na mtukuze ukimhimidi. Na inamtosheleza kuwa ni Mjuzi wa khabari za dhahiri na za siri kuhusu dhambi za Waja Wake. Ambaye ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake ndani ya siku sita, kisha akalingana juu ya ‘Arshi. Mwingi wa rehema, basi ulizia kuhusu Yeye, kwani ni Mjuzi wa khabari za dhahiri na za siri!”[5]

Je, kuna yeyote awezaye kukanusha chochote katika sifa hizi zinazofahamisha ukamilifu na utukufu?

6 – Amesema sehemu ya sita katika ”as-Sajdah”:

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۚ بَلْ هُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ مَا لَكُم مِّن دُونِهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا شَفِيعٍ ۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ذَٰلِكَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ

”Au wanasema ameitunga? Bali hiyo ni haki kutoka kwa Mola wako ili uonye watu ambao hawakufikiwa na mwonyaji yeyote kabla yako, huenda wakaongoka. Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake ndani ya siku sita, kisha akalingana juu ya ‘Arshi. Nyinyi hamna badala Yake mlinzi yeyote wala mwombezi. Je, basi hamkumbuki? Anadabiri mambo kutoka mbinguni mpaka ardhini, kisha inapanda Kwake katika siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu katika ile mnayoihesabu nyinyi. Huyo Ndiye Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.”[6]

Je, kuna yeyote awezaye kukanusha chochote katika sifa hizi zinazofahamisha ukamilifu na utukufu?

7 – Amesema sehemu ya saba katika ”al-Hadiyd”:

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

“Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho na Aliye juu na Aliye karibu – Naye juu ya kila jambo ni mjuzi. Yeye ndiye aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ‘Arshi; anajua yale yanayoingia ardhini na yale yatokayo humo na yale yanayoteremka kutoka mbinguni na yale yanayopanda humo – Naye yupamoja nanyi popote mlipo. Allaah ni Mwenye kuyaona yote myatendayo.”[7]

Manhaj wa Diraasaat li Aayaat-il-Asmaa’ was-Swifaat, uk. 104-107

[1] 7:54

[2] 10:3-6

[3] 13:2-4

[4] 20:1-8

[5] 25:58-59

[6] 32:3-6

[7] 57:3-4

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 19-22
  • Imechapishwa: 27/11/2025