al-Hasan (Rahimahu Allaah) amesema:
“Kuna aina mbili ya elimu. Elimu ya kwenye ulimi. Elimu hiyo ni hoja ya Allaah dhidi ya mwanadamu. Nyingine ni elimu ya kwenye moyo. Hiyo ndiyo elimu yenye manufaa.”
Imepokewa pia kutoka kwa al-Hasan kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) pasi na Swahabah katika cheni ya wapokezi. Ameipokea vilevile kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kupitia kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Hata hivyo cheni hizo zilizoungana hazikusihi.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akakhabarisha kuwa elimu ya watu wa Kitabu iko ndani ya vitabu vyao, lakini hawanufaiki na chochote katika hayo baada ya kupoteza malengo yake. Malengo yake ni kule kuisoma kwao kufike ndani ya nyoyo zao ili wapate utamu wa imani na kunufaika nayo kwa kupata khofu na kutubia. Kuwa nayo kwenye ulimi peke yake ni hoja dhidi yao.
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 46-48
- Imechapishwa: 24/11/2025
al-Hasan (Rahimahu Allaah) amesema:
“Kuna aina mbili ya elimu. Elimu ya kwenye ulimi. Elimu hiyo ni hoja ya Allaah dhidi ya mwanadamu. Nyingine ni elimu ya kwenye moyo. Hiyo ndiyo elimu yenye manufaa.”
Imepokewa pia kutoka kwa al-Hasan kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) pasi na Swahabah katika cheni ya wapokezi. Ameipokea vilevile kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kupitia kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Hata hivyo cheni hizo zilizoungana hazikusihi.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akakhabarisha kuwa elimu ya watu wa Kitabu iko ndani ya vitabu vyao, lakini hawanufaiki na chochote katika hayo baada ya kupoteza malengo yake. Malengo yake ni kule kuisoma kwao kufike ndani ya nyoyo zao ili wapate utamu wa imani na kunufaika nayo kwa kupata khofu na kutubia. Kuwa nayo kwenye ulimi peke yake ni hoja dhidi yao.
Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 46-48
Imechapishwa: 24/11/2025
https://firqatunnajia.com/9-elimu-ya-kwenye-ulimi-elimu-ya-kwenye-moyo/