Swali 85: Ni sababu zipi zinazopelekea katika kukusanyika?
Jibu: Mosi ni kwamba umoja unapatikana kwa kuisahihisha ´Aqiydah kwa njia ya kwamba inakuwa yenye kusalimika kutokana na shirki. Amesema (Ta´ala):
وَإِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ
”Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja Nami ni Mola wenu. Hivyo nicheni.”[1]
Kwa sababu ´Aqiydah sahihi ndio inayozifanya nyoyo kuungana na kuondoa kinyongo, tofauti na pindi I´tiqaad na waungu wanakuwa wengi. Katika watu wa kila ´Aqiydah wanashikilia ´Aqiydah na mungu wao na huona vyengine vyote ni batili. Allaah (Ta´ala) amesema:
أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ
“Je, miola wengi wanaofarakana ni bora au Allaah Mmoja pekee, Mwenye kudhibiti na kudhalilisha?”[2]
Kwa ajili hiyo waarabu katika kipindi kabla ya kuja Uislamu walikuwa wametawanyika na wanyonge. Wakati walipoingia katika Uislamu na wakazirekebisha ´Aqiydah zao, ndipo wakawa na umoja na nchi yao ikawa moja.
Pili kumsikiliza na kumtii mtawala wa waislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Nakuamrisheni kumcha Allaah (´Azza wa Jall) na kusikiliza na kutii hata kama mtatawaliwa na mja wa kihabeshi.”[3]
Kwa sababu kumuasi mtawala ni sababu ya tofauti.
Tatu ni kurejea katika Qur-aan na Sunnah katika kutatua migogoro na tofauti. Amesema (Ta´ala):
فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا
”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[4]
Watu wasirejee katika maoni na desturi za wanamme.
Nne ni kusuluhisha ile mizozo inayotokea kati ya watu. Amesema (Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ
”Basi mcheni Allaah na suluhisheni yaliyo kati yenu na mtiini Allaah na Mtume Wake mkiwa ni waumini.”[5]
Tano ni kuwapiga vita waasi na Khawaarij. Wao ndio wanaotaka kuwafanya waislamu kugawanya. Pale tu wanapokuwa na nguvu basi wanatishia jamii ya Kiislamu na kuiharibu amani yake. Amesema (Ta´ala):
فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ
”Lakini mojawapo likikandamiza jengine, basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee katika amri ya Allaah.”[6]
Kwa ajili hiyo ndio ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) maana akawapiga vita waasi na Khawaarij, jambo ambalo linazingatiwa ni moja katika sifa zake.
[1] 23:52
[2] 12:39
[3] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2776) na al-Haakim (1/96) na tamko ni lake.
[4] 4:59
[5] 8:1
[6] 49:9-10
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 211-213
- Imechapishwa: 24/07/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 211-213
Imechapishwa: 24/07/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/85-ni-vipi-waislamu-watakuwa-na-umoja/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)