82. Je, kunahitajika kwanza kupata idhini kutoka kwa mtawala kwa ajili ya Qunuut?

Swali 82: Je, kunahitajika kwanza kupata idhini kutoka kwa mtawala kwa ajili ya Qunuut?

Jibu: Swalah ni ´ibaadah na kwa ajili hiyo haifai kuingiza kitu ndani yake isipokuwa baada ya fatwa kutoka kwa wanazuoni. Wanatakiwa kulidurusu suala hilo na kukadiria ni lini inafaa kusoma Qunuut na ni lini haifai kuisoma. Haijuzu kuleta vurugu ndani ya swalah. Ikitoka fatwa kutoka kwa wanazuoni ya kusoma Qunuut, hapo ndipo mtawala ataieneza fatwa hii kwa watu. Vinginevyo imamu hatakiwi kusoma Qunuut.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 209
  • Imechapishwa: 23/07/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy