Ama roho yenye giza, yenye uchafu na yenye ukakasi, basi haifunguliwi milango ya mbingu wala haipaishwi kwa Allaah (Ta´ala). Bali hurudishwa kutoka mbingu ya chini kwenda kwenye ulimwengu wake na chanzo chake. Kwa sababu hiyo ni ardhi ya chini, na ile ya kwanza ni ya juu ya mbinguni. Basi kila roho hurudi katika asili yake na kile ilichotokana nacho, jambo ambalo limebainishwa katika Hadiyth ndefu ya al-Baraa bin ´Aazib (Radhiya Allaahu ´anh) ambayo imepokelewa na Imaam Ahmad, Abu ´Awaanah al-Isfaraayiyniy katika ”as-Swahiyh” yake, al-Haakim na wengineo. Nayo ni Hadiyth Swahiyh.
Makusudio ni kuwa Allaah (´Azza wa Jall) hakipandi Kwake miongoni mwa matendo, maneno na roho isipokuwa kile kilicho kuwa nuru. Walio karibu zaidi Naye na waenziwa zaidi mbele Yake ni wao. ´Abdullaah bin ´Amr ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amewaumba viumbe Vyake katika giza. Kisha akawatupia miongoni mwa nuru Yake. Basi yule aliyepata nuru hiyo huongoka na yule mwenye kuikosa hupotea. Kwa ajili hiyo nasema kuwa kalamu imekwishakauka kwa mujibu wa utambuzi wa Allaah (´Azza wa Jall).”[1]
Hadiyth hii tukufu na ni msingi miongoni mwa misingi ya imani na pia hufunguka kupitia hiyo mlango mkubwa wa siri ya makadirio na hekima yake.
Hiyo nuru aliyowatupia ni ile iliyowahuisha na kuwaongoza, ambapo maumbile yakapokea na kupata sehemu yake. Lakini kwa kuwa haikutosha kwa ukamilifu wake, ndipo akawakamilishia na kuwahitimishia kwa roho aliyoipeleka kwa Mitume Wake (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na kwa nuru aliyowateremshia nayo kama wahy. Basi maumbile yakakusanya nuru ya kwanza iliyotupwa katika ile nuru ya wahy na ya kinabii. Nuru juu ya nuru! Basi nyoyo zikaangaza, nyuso zikaangazwa, roho zikahuishwa na viungo vikajisalimisha kwa utiifu, kwa khiyari na kwa kutaka mwenyewe. Hivyo basi uhai wa moyo pia ukatiwa nguvu.
[1] Ahmad (2/176), at-Tirmidhiy (2642), ambaye amesema kuwa ni nzuri, Ibn Abiy ´Aaswim (242-243) na al-Haakim (1/30), aliyeisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Swahiyh na nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (242-243).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 145-149
- Imechapishwa: 01/09/2025
Ama roho yenye giza, yenye uchafu na yenye ukakasi, basi haifunguliwi milango ya mbingu wala haipaishwi kwa Allaah (Ta´ala). Bali hurudishwa kutoka mbingu ya chini kwenda kwenye ulimwengu wake na chanzo chake. Kwa sababu hiyo ni ardhi ya chini, na ile ya kwanza ni ya juu ya mbinguni. Basi kila roho hurudi katika asili yake na kile ilichotokana nacho, jambo ambalo limebainishwa katika Hadiyth ndefu ya al-Baraa bin ´Aazib (Radhiya Allaahu ´anh) ambayo imepokelewa na Imaam Ahmad, Abu ´Awaanah al-Isfaraayiyniy katika ”as-Swahiyh” yake, al-Haakim na wengineo. Nayo ni Hadiyth Swahiyh.
Makusudio ni kuwa Allaah (´Azza wa Jall) hakipandi Kwake miongoni mwa matendo, maneno na roho isipokuwa kile kilicho kuwa nuru. Walio karibu zaidi Naye na waenziwa zaidi mbele Yake ni wao. ´Abdullaah bin ´Amr ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amewaumba viumbe Vyake katika giza. Kisha akawatupia miongoni mwa nuru Yake. Basi yule aliyepata nuru hiyo huongoka na yule mwenye kuikosa hupotea. Kwa ajili hiyo nasema kuwa kalamu imekwishakauka kwa mujibu wa utambuzi wa Allaah (´Azza wa Jall).”[1]
Hadiyth hii tukufu na ni msingi miongoni mwa misingi ya imani na pia hufunguka kupitia hiyo mlango mkubwa wa siri ya makadirio na hekima yake.
Hiyo nuru aliyowatupia ni ile iliyowahuisha na kuwaongoza, ambapo maumbile yakapokea na kupata sehemu yake. Lakini kwa kuwa haikutosha kwa ukamilifu wake, ndipo akawakamilishia na kuwahitimishia kwa roho aliyoipeleka kwa Mitume Wake (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na kwa nuru aliyowateremshia nayo kama wahy. Basi maumbile yakakusanya nuru ya kwanza iliyotupwa katika ile nuru ya wahy na ya kinabii. Nuru juu ya nuru! Basi nyoyo zikaangaza, nyuso zikaangazwa, roho zikahuishwa na viungo vikajisalimisha kwa utiifu, kwa khiyari na kwa kutaka mwenyewe. Hivyo basi uhai wa moyo pia ukatiwa nguvu.
[1] Ahmad (2/176), at-Tirmidhiy (2642), ambaye amesema kuwa ni nzuri, Ibn Abiy ´Aaswim (242-243) na al-Haakim (1/30), aliyeisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Swahiyh na nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (242-243).
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 145-149
Imechapishwa: 01/09/2025
https://firqatunnajia.com/80-nuru-juu-ya-nuru/