Elimu yenye manufaa inakuwa ndani ya nyoyo na kuwapa utulivu, khofu, staha mbele ya Allaah, unyenyekevu na kujivunjavunja. Ikiwa elimu kama hiyo haipatikani moyoni, na ikawa iko tu kwenye ulimi, basi ni hoja ya Allaah dhidi ya mwanadamu – inakuwa dhidi ya mwenye nayo na wengineo. Kama alivosema Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anh):

“Kuna watu wanaosoma Qur-aan bila kuvuka mitulinga yao. Lakini inamnufaisha mwenye nayo pale tu inapotua na kukita ndani ya moyo.”

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 47
  • Imechapishwa: 24/11/2025