Fungu la tatu ambao ndio viumbe wenye khasara zaidi. Nao ni wale ambao hawakukubali uongofu wa Allaah na wala hawakukipa umuhimu. Kwa msemo mwingine hawana kuhifadhi, kufahamu, kusimulia, uelewa, faida.

Fungu la kwanza ni wale watu wenye kusimulia, faida na uelewa.

Fungu la pili ni wale watu wenye kusimulia na wenye faida na pia wanayo sehemu ya uelewa ingawa sehemu yao ya kuhifadhi ndio kubwa zaidi.

Fungu la tatu ni wale watu waliokula khasara na hawana kusimulia, uelewa wala faida:

إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا

”Si vyenginevyo isipokuwa ni kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia!”[1]

Hawa ndio wanaofanya maisha yawe mafupi na hufanya bei kupanda. Hakuna wanachojali isipokuwa matumbo na tupu zao. Ikiwa hamu yake itapanda juu kidogo, basi itakuwa bado inazunguka katika mavazi yake na mapambo yake. Iwapo hamu yake itapanda juu ya hayo, basi itakuwa katika kutafuta uongozi na ushindi kwa ajili ya nafsi yenye ghadhabu. Iwapo itainuka juu zaidi kutoka katika kutetea nafsi ya ghadhabu, basi hamu yake itakuwa katika kutetea nafsi ya mbwa na haikuridhika hadi kutetea nafsi ya mnyama wa mwituni. Hakuna yeyote kati yao aliyekirimiwa. Hakika nafsi zina aina mbalimbali:

1 – Nafsi ya mbwa.

2 – Nafsi ya mnyama wa mwituni.

3 – Nafsi ya kifalme.

Nafsi ya mbwa huridhika na mfupa, kipande cha chakula, mzoga na uchafu.

Nafsi ya mnyama wa mwituni haiwezi kuridhika na hayo; bali inataka kushinda nafsi zingine kwa nguvu na inataka kutawala juu ya wengine kwa haki au batili.

Nafsi ya kifalme basi imeinuka juu ya hayo na imenyanyuka kuelekea kwa rafiki wa juu kabisa. Hamu yake ni elimu, imani, kumpenda Allaah (Ta´ala), kurejea Kwake, kuipa kipaumbele mapenzi Yake na radhi Zake. Huchukua kutoka ulimwengu kile kinachomsaidia kufikia kwa Muumbaji wake, Mola na Mlinzi wake, siyo kujifungamanisha nacho kutokamana Naye.

[1] 25:44

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 141-142
  • Imechapishwa: 27/08/2025